Pichani
Kutoka kushoto ni Bella Kombo akiongoza mashambulizi ya jukwaa akipewa
sapoti na Digna Mbepera(katikati) na kwa mbaliiiii ni Aneth kushaba.
Aneth
Kushaba AK 47 akizipiga vocal za kutoshaaaa ili kuwapa burudani wapenzi
wa Skylight Band ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita.
Bella Kombo akitia madaha yake na swagga kibao ndani ya Thai Village.
Digna Mbepera (Mtoto Mzuri) akiimba kwa hisia kali kuwapa ladha wapenzi wa Skylight band ndani ya Thai Village
Anaitwa Hashimu Donode mkali wao akizipiga zile vocal kaliiii na tamuuu kuwapa raha mashabiki wake ndani ya Thai Village
Wanamwita
tamu ya warembo au Sukari ya warembo si mwingine ni Sam Mapenzi
akizipiga zile Vocal lainiii za taratibu kuwapa raha mashabiki wake
ndani ya Thai Village
Le
Meneja Her Self Aneth Kushaba AK 47 akiongoza Skylight Divas
kuporomosha burudani ya nguvuuuu ndani ya Thai Village,Usikose raha hizi
leo.
Muziki
ni hisia na hapa ndicho anachokifanya Aneth Kushaba hebu mtazame
anavyoimba kwa hisia kali na Vitendo ili kuwapa raha mashabiki wake huku
akipewa sapoti kwa mbaliiii na Digna Mbepera(katikati) na Bela Kombo wa
mwisho kushoto.
Majembeeee(vijana wa kazi)wakilishambulia Jukwaa vilivyo.
Mikono kichwaniii,ahhh ahhhh majembe ya Skylight wakishambulia jukwaa kwa nguvuuuu.
Joniko Flower baba ya congo akiongoza kushambulia huku akipewa sapoti na Sony Masamba(katikati) pamoja na Sam Mapenzi.
Mtia
ladhaa mahiri wa Skylight akiwa anasahangaa kupata Ukodak kutoka kwa
mpiga picha wetu,Huku mpiga drums Idrisa akichunguliaaa kwa mbaliiiii.
Huyu jamaa ni muhimu sanaaa ndani ya Sklight Band anaitwa Daudi Tumba,akizipiga Tumba zake lazima ufurahie.
Sam
mapenzi (wa kwanza kulia) akiimba kwa upoleeeee kabisaaaa huku akipewa
sapoti na Aneth Kushaba(katikati)na Digna Mbepera wa kwanza kushoto.
Yani
weweee unanipaaa raahaaa sana ukiwa unaimbaaaa ni shabiki huyu
akionyesha mapenzi ya kutoshaaaa kwa Hashimu Donode baada ya kukunwa na
uimbaji wake.
Joniko Flower baba ya Congo akiongoza Vijana wake kushambulia jukwaaaa.
Sony masamba(katikati) akikamuaaaa sebeneee sebeneeee kwa nguvuu zoteeee.
Kama
kawaida Skylight Band inavyowapenda mashabiki wake huwa kila Ijumaa
shabiki anayesheherekea siku yake ya kuzaliwa hupewa nafasi ya kuimbiwa
special Song na kusheherekea na mashabiki wake,Hahahaha si unaona
mwenyeweeee hapoooo.
Hapo sasa ni viuno, mabega, mikono inahusika kuweza kuyarudi.
Nyomiiiii la mashabikiiii wakifurahia muziki mzuriiiii.
Kama una furahaaa mikonooo juuuu juuuuuuu.
Kikuku
huyoooooo.....ana maringooo huyoooo...kwioooo kwiooooo..... Iyo
inaitwaga kikukuu ni staili yenye rahaaaaa na utamu unapochezeshwa na
Skylight Band.
Hiyo staili inaitwaaa sugua suguaaa achaaa ni hatariiiiiiiiii.
Mratibu wa Skylight Band Rubeya akishow Love na Mashabiki ndani ya Thai Village.
Sam Mapenzi akipata Ukodak na Shabiki wake.
Hashimu Donode akipata Ukodak na Mashabiki wake.
Skylight band Divas wakifurahia kuapata Ukodak mbele ya kamera yetu.
Kama kawaida yetu inapofika mwishoni mwa juma yaani Ijumaa huwa
inakuwa ni siku ya furaha na kubadilishana mawazo, kupunguza stress za
kazini.....paleee Thai Village Masaki.Kwenye Jukwaa Bendi yako matata na
inayotikisa Tanzania na Jiji la Dar Skylight Band wanakuwa wanakupa
burudani ya nguvu na iliyoenda shule.Karibu leo kuanzia saa 3 kamili
usiku upate zile Afropop, Zouk, Lingala,Sebene, Reggae, Naija Flava na
zingine kibao!