Staa wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, akiwa na mpenziwe Nuh Mziwanda.
“Mimi ninampenda Shilole kwa asilimia 100, ila siko tayari kubadili
dini kwa ajili yake maana kwetu ni wakristo na hapa naongea mama yangu
ni mzee wa kanisa hivyo Shilole naamini anaweza kubadili maana mimi
tayari nimeshafanya mengi sana juu yake.”
Zuwena Mohamed ‘Shilole’, na mpenziwe Nuh Mziwanda wakipozi.
Msikie Shilole: Mimi siwezi kubadili dini maana Nuh ndiye alisema
atabadili hata hivyo familia yangu haiwezi kunikubalia kubadili dini kwa
ajili ya kufunga ndoa kama amesema naye hawezi kubadili basi tutaishi
tu maana hata ndoa ya serikali yenyewe hawezi na maisha siyo lazima
tuoane.”