
Msanii
wa Kundi la Orijino Komedy, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’
(katikati) akielezea jinsi kundi lake litakavyofanya makamuzi kwenye
tamasha hilo. Kushoto ni Isaya Mwakilasa ‘Wakuvanga’ na Lukas Mhuvile
‘Joti’, kulia ni Meneja wa Bidhaa za Tigo, Edwin Mgoha na msanii wa
muziki wa kizazi kipya, Farid Kubanda ‘Fid Q’.

Meneja wa Bidhaa za Tigo akisistiza jambo.

Masanja Mkandamizaji akilonga na wanahabari (hawapo pichani).

Wanahabari wakiwa kazini.

Msanii
wa Orijino Komedy, Mujuni Silvery ‘Mpoki’ (kulia) akiahidi kufanya
makuu kwenye tamasha hilo. Kulia ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya,
Mwana FA akifuatiwa na Mac Reagan wa Orijino Komedy.

Mac Reagan akijaribu kuonesha mambo anayotarajia kwenda kuyafanya kwenye tamasha hilo.

Masanja Mkandamizaji, Wakuvanga (kushoto) na Joti (aliyesimama) wakionesha mbwembwe zao.

Joti na Young Killer wakiwa kwenye pozi.
KUNDI la vichekesho la Orijino Komedy kwa
kushirikiana na wanamuziki wa kizazi kipya akiwemo, Farid Kubanda ‘Fid
Q’ na Young Killer, keshokutwa Jumamosi wanatarajia kutoa burudani ya
nguvu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwenye tamasha liitwalo
Welcome Pack ambalo limeandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika leo katika ofisi
za Tigo zilizopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bidhaa za
Tigo, Edwin Mgoha, alisema katika tamasha hilo kiingilio kitakuwa ni
laini ya tigo ambapo wateja watakaofika watapata maelekezo ya huduma
mbalimbali za mtandao huo.
(PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL)