Stori: Imelda Mtema
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda
amefunguka kuwa watu wanaomsema vibaya kuhusu yeye kupewa kichapo na
mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wanakosea kwani anaamini kufanywa
hivyo ni mahaba.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii
hivi karibuni, Mziwanda alisema kuna taarifa zimeenea kuwa huwa anapigwa
na Shilole pindi anapokosea lakini ukweli si kupigwa ‘live’ bali ni
kupigwa kimahaba.
“Jamani kupigwa wanakozungumzia watu
sielewi lakini mimi ananipiga kimahaba, wanaosema kuwa mpenzi wangu
ananipiga washindwe, watuache kwa raha zetu,” alisema Shilole.
