Kituo
cha Kisasa cha Uchunguzi na Matibabu ya magonjwa ya binadamu
kinachojengwa katika Chuo Kikuuu cha Dodoma (UDOM) kikiwa katika hatua
za mwisho mwisho za kukamilika.
Kituo
hiki kitahudumia wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya jirani
ya na mkoa wa Dodoma na kinajengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya NHIF kwa gharama ya shilingi Bilioni 36 ambazo zimetolewa
na mfuko huo kwa silimia 100.
Akizungumza
na wahariri wa vyombo mbalimbali wanaohudhuria kongamano la Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya linalofanyika kwenye hoteli ya Dodoma mjini humo
walipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Kaimu
Mkuu wa Chuo hicho Profesa Mlacha Shaaban amesema “Kituo hiki
kitajikita zaidi kwenye magonjwa ya uchunguzi na utafiti pia kitatoa
wataalamu kutoka katika kitivo cha afya cha Chuo kikuu cha UDOM na
wataalamu watakaofanya kazi katika kituo hicho watakuwa wakifundisha
wanafunzi na kuhudumia wagonjwa. Kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutoa
huduma ifikapo Januari 2015"
Jengo la kituo cha Utafiti na tiba cha UDOM kinachojengwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF.
Kaimu
Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha UDOM Profesa Mlacha Shaaban akizungumza
na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali walipotembelea ujenzi wa
kituo cha Tiba na Utafiti kinachojengwa katika chuo kikuu cha UDOM.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamotoakizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo hicho
Waandishi wa habari wakisubiri kupata maelezo ya kituo hicho.
NA MICHUZI JR