Mkuu wa Wilaya Ahmed Kipozi Aiba Mifuko 700 ya Saruji
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Bw Ahmed
Kipozi ameiba jumla ya mifuko 700 ya sementi aliyokabidhiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Pwani, Bi Mwantumu Mahiza. Akizungumza kwenye kikao cha baraza
la madiwani jana, Bi Mahiza alidai kwamba alimpa Kipozi jumla ya mifuko
1000 ya sementi kwa ajili ya ujenzi wa shule lakini Bw Kipozi alitumia
mifuko 300 tu huku akiiba mifuko 700 na kuipeleka kusikojulikana.
Kipozi amepewa siku 2 (masaa 48) awe
amerudisha mifuko hiyo aliyoiba vinginevyo cha moto atakiona. Haikuweza
kufahamika mara moja ikiwa mtuhumiwa huyo atashindwa kurudisha sementi
hiyo aliyoiba atachukuliwa hatua gani.
Source: RFA/Jamii Forums