Mbunge
wa kuteuliwa, James Mbatia akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya
Bishop Moshi, Sophia Mushi na viongozi wengine wa shule hiyo wakati
alipotembelea mazingira ya shule hiyo.
Mhe.
Mbatia akitizama moja ya chumba katika bweni la wasichana la Shule ya
Sekondari Bishop Moshi , chumba ambacho kimewekewa miundombinu mizuri
ikiwemo milango kila mahali jambo ambalo linasaidia pindi kunapotokea
majanga yakiwemo ya moto.
Mbatia
akizungumza jambo mara baada ya kuingia katika chumba maalumu cha
kujifunzia Kompyuta na kukuta bado shule hiyo wanatumia komputa
zilizopitwa wakati.
Mbatia akitizama baadhi ya vitabu katika maktaba ya shule hiyo, kulia ni mkuu wa shule hiyo, Sophia Mushi.
Mbatia akitizama bweni la wavulana baada ya kutembelea shuleni hapo.
(Picha na Michuzi Blog)