Mwenyekiti
Mtendaji wa Kampuni ya Petrogas inayojihusisha na kutoa mafunzo kwa
ajili ya uandaaji wa mapendekezo ya miradi pamoja na usimamizi wake
yenye makazi yake jijini Dar es Salaam Bw. Greyson Kiondo akisisitiza
jambo kwenye mafunzo yanayohusu uandaaji wa mapendekezo ya miradi na
usimamizi wake yaliyoshirikisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na
Madini yanayoendelea mjini Bagamoyo katika hoteli ya Stella Maris.
Msimamizi
wa mradi unaohusika na kuwajengea uwezo wataalamu wa nishati na
tasnia ya uziduaji (CADESE; Capacity Development in the Energy Sector
& Extractive Industries) Bw. Paul Kiwele (kulia) akisisitiza jambo
kwenye mafunzo hayo. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi
Innocent Luoga.
Kamishna
Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga ( wa kwanza kulia mbele ),
msimamizi wa mradi wa CADESE Bw. Paul Kiwele (katikati) na baadhi ya
washiriki wakiendelea kufuatilia mada iliyokuwa inawasilishwa na
mtaalamu mwelekezi Bw. Tom Mitro kutoka Petrogas (hayupo pichani).
Mtaaalamu
kutoka Petrogas Bw. Tom Mitro akiwasilisha mada juu ya uandaaji wa
mapendekeo ya miradi katika semina hiyo mbele ya washiriki (hawapo
pichani).
Kamishna
Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) akisoma hotuba ya
ufunguzi kwa niaba ya Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli
Mhandisi Hosea Mbise kwenye mafunzo hayo. Kulia ni msimamizi wa mradi wa
CADESE Bw. Paul Kiwele.
CHANZO MICHUZI BLOG