Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP),
Leonard Paul (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mshauri wa
Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira (kushoto) na Mshauri wa
Kampuni ya Mabibo, Kamala Stephen baada ya kufungua semina hiyo katika
Hoteli ya Top Life mjini Morogoro.
Mshauri
wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira (katikati),
akizungumza katika semina hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma wa
Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi (ACP), Ali Ali na Ofisa Mwandamizi wa
Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkunga Tuwaha.
Maofisa
wa polisi ambao ni mameneja katika Kantini za jeshi hilo kutoka mikoa
ya Njombe, Tanga, Dodoma, Morogoro, Tanga na Dar es Salaam wakiwa kwenye
senina hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi (ACP), Ali Ali (kushoto), akichangia mada katika semina hiyo.
Ofisa
Mwandamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkunga Tuwaha
(kulia), akitoa ufafanuzi kuhusu msamaha ya kodi kwenye maduka ya
polisi.
Ofisa Mwandamizi wa Kodi wa TRA, Mgaya Mussa Faraji
akitoa ufafanuzi mbalimbali kuhusu kodi.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Ramadhan Abdul Mambea (kulia), naye akichangia jambo kwenye semina hiyo.
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Bia ya Mabibo, Eustadius Mutabingwa (kulia), naye alichangia uzoefu wake katika semina hiyo.
Mkurugenzi
wa Maghala na Usalama wa Kampuni ya Mabibo Bia (MBL), Boniface
Katanyebile naye alikuwa katika semina hiyo akifuatilia kila jambo
lililokuwa likijadiliwa.
Wadau wakiwa katika semina hiyo.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Bia ya Mabibo (MBL), Respicius Didace akitoa historia
fupi ya kampuni ya Mabibo na mambo mbalimbali ya kisheria kuhusu utii wa
sheria bila shuruti.
Ofisa
Mnadhimu wa Jeshi la Polisi, SSP Gemin Mushy (kushoto) na Mshauri wa
Kampuni ya Mabibo, Kamala Stephen wakifuatia mada katika semina hiyo.
Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema ni kosa
kisheria kwa mtu kukutwa akiuza bidhaa au vinywaji vilivyosamehewa kodi
na serikali vinavyouzwa majeshini.
Hayo yalisemwa na Ofisa Mwandamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Mkunga Tuwaha wakati akitoa mada kwenye semina
shirikishi kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Bia ya Mabibo
iliyofanyika Top Life Hoteli mjini Morogoro leo asubuhi iliyohusu
kujadili mambo mbalimbali ya jeshi hilo na utii wa sheria bila shuruti.
"Vinywaji na bidhaa zingine zenye msamaha wa kodi hasa katika
majeshi yetu ni vema zikatumika kwa ajili ya askari na familia zao na si
mtu mwingine" alisema Tuwaha.
Alisema kumekuwa na baadhi ya askari wasio waaminifu wamekuwa
wakitoa vitambulisho vyao na kuwapa watu wengine kwa ajili ya kwenda
kununua bidhaa mbalimbali kwenye maduka ya majeshini yenye msamaha wa
kodi jambo ambalo ni kwenda kinyume.
Alisema bidhaa na huduma zilizosamehewa kodi ya ongezeko la thamani (VAT), zinatajwa katika kifungu namba 10 kikisomwa pamoja na jedwali la pili la sheria ya VAT, sura 148.
Alitaja baadhi ya bidhaa hizo ni kama mifugo, mazao ya nyama kama iliyosindikwa, mazao ya maziwa, samaki na mazao ya kilimo.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea Fr James Rugemalira alilishukuru jeshi la polisi kwa ushirikiano linao hutoa katika shughuli mbalimbali kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi kwani bila ya jeshi hilo amani inaweza kutoweka na wananchi wakashindwa kufanya shughuli zao mbalimbali za uzarishaji mali.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Mabibo Respicius Didace alisema ni vizuri kila mtu akajenga tabia ya kutia sheria bila ya kuingilia haki ya mtu mwingine kazi ambayo inayosimamiwa na jeshi la polisi.
Mshauri wa Kampuni hiyo Kamala Stephen alisema uingiza wa Bia za Windhoek Lager nchini kutoka Afrika Kusini ni kukiuka taratibu kwani anayepaswa kuuza bia hizo katika soko la Tanzania ni Kampuni ya Bia ya Mabibo na si vinginevyo.
Alisema ukitaka kuitambua bia za Windhek ambazo ni halali ubavuni mwa chupa kuna namba MB66 na inatengenezwa na Kiwanda cha Bia cha Namibia.
Semina hiyo ilishirikisha askari wa jeshi hilo ambao ni mameneja wa kantini kutoka mikoa ya Njombe, Tanga, Dodoma, Morogoro, Tanga na Dar es Salaam na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Mabibo. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)