Mbunge
wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akizungumza na vikundi
mbalimbali mbalimbali vya Joging vilivyoshiriki katika tamasha la Mbio
za Amani lililoshirikisha wawakilishi kutoka pande mbalimbali za nchi na
kupokelewa na mbunge huyo ambye alikuwa mgeni rasmi, Dr. Khamis
Kigwangala amewaasa wanasiasa kutoleta siasa za uchochezi hasa katika
mchakato mzima wa Katiba mpya ambapo amesema waachwe wananchi wenyewe
waisome waielewe na wao wataamua kama wataipigia kura ya Ndiyo au
Hapana, mapokezi hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es salaam leo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akishiriki katika zoezi la viungo mara baada ya kupokea vikundi hivyo vya Jogging kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akipokea vikundi vya Jogging katika viwanja vya Mnazi Mmoja mara baada ya kumaliza mbio za Amani.
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akipokea vikundi vya Jogging katika viwanja vya Mnazi Mmoja mara baada ya kumaliza mbio za Amani.
Bw.Abdulla
Mohamed Mwenyekiti wa Mipango ya Maandalizi ya tamasha hilo akimkabidhi
jenzi Mwenyekiti wa Barza la Michezo BMT Bwa Dioniz Malinzi.
Mdau wa michezo na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Kanali Mstaafu Iddi Kipingu akizungumza na vikundi hivyo.
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akishiriki kuchezo kigoma cha Amani mara baada ya kupokea vikundi vya Jogging katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Bw.
Dioniz Malinzi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo BMT akizungumza jambo na
vikundi hivyo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Tamasha la Mbio
za Amani.
Vikundi hivyo vikifanya mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Vikundi hivyo vikiimba wimbo wa Taifa.
.......................................................................
Wanasiasa
wameaswa kudumisha amani, upendo na mshikamano wa Tanzania, ili kuepuka
vurugu zinazoweza kujitokeza ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa
zikisababishwa na makundi ya wanasiasa, kwa kutoa ujumbe kwa wananchi
unao chochea kuvurugukika kwa amani ya Tanzania.
Akizungumza
na wanamichezo wa vilabu mbalimbali vya kukimbia (Jogging) kutoka
Tanzania bara na Zanzibar, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam, mbunge wa jimbo la Nzega, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya
bunge ya Tawala za mikoa na seikali za mitaa, Dk. Hamis Kigwangala,
amesema wakati bunge maalum la Katiba lilipokuwa likitunga katiba
inayopendekezwa, kuliibuka baadhi ya wanasiasa, waliokana kushiriki
katika bunge hilo na kutofautiana katika baadhi ya mambo kuingizwa
katika katiba hiyo, huku wale waliobaki ndani ya bunge maalumu la katiba
kwa asilimia takriban 85 wakiheshimu maamuzi ya watanzania na
kuhakikisha katiba mpya inapatikana.
Hivyo
amewataka wanasiasa pamoja na kuwa mapendekezo yao hayakuingia ndani ya
katiba wasiwe chanzo cha kutokuridhika kwao kulazimisha na watanzania
wengine wasiridhike na kwamba watanzania waachwe siku ya kuipigia kura
katiba inayopendezwa itakapo tangazwa, watanzania waipigie kura ya ndio
au hapana na kwamba waamue kwa utashi wao bila uchochezi wa wanasiasa.
Katika
Tamasha hilo lililopewa jina la Mbio za amani 2014, Dk, Kigwangala pia
amehimiza umuhimu wa kufanya michezo kila wakati, kwani michezo ni Afya,
Furaha, Amani, Upendo na Ajira, huku akivitunuku vyeti baadhi ya vilabu
vya Jogging kwa kushiriki katika tamasha hilo.
Tamasha
hilo limeshirikisha wanamichezo wa vilabu vya Jogging kutoka Zanzibar,
Dodoma na Dar es Salaam, ambapo limeandaliwa na Faita Jogging &
Sports Club ya jijini Dar es Salaam, huu ukiwa ni mwaka wa tatu
kuandaliwa.