Oct 30, 2014

UFUNGUZI WA KONGAMANO LA TANO LA JOTOARDHI

 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (wa pili kushoto) akimwongoza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,   Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa pili kulia) kutoka eneo la mkutano katika Ukumbi wa Mikutano wa  Kimataifa AICC mara baada ya ufunguzi wa
Kongamano la Tano la Kimataifa ambalo linajadili masuala mbalimbali kuhusu matumizi ya nishati ya jotoardhi kwa nchi wananchama  kwa nchi zilizo katika bonde la ufa na nchi nyingine duniani.  Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo na Mkurugenzi wa
Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Julius Ningu (wa kwanza kulia).
 Sehemu ya Washiriki wanaohudhuria Kongamano la tano la Kimataifa la Jotoardhi kwa nchi zilizo katika bonde la Ufa katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa  wakifuatilia hotuba ya  ufunguzi kutoka  kwa Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.  Mohamed Gharib Bilal (katikati) akifuatilia taarifa kuhusu Kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi, wengine kutoka kushoto ni Kamishna wa Miundombinu na Nishati kutoka Umoja wa Nchi za Afrika Dkt. Elham Ibrahimu, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava, Naibu wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Stephen Masele, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira kwa Ukanda wa Afrika (UNEP), Mounkaila Goumandakoye, Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya nishati wa Iceland Einar Gunnarsson na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Gharib Mohamed Bilal mara baada ya kufungua Kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi.

 Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi katika picha ya Pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal baada ya kufungua kongamano hilo.
 Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Nishati, Einar Gunnarsson akitoa taarifa kwa ufupi kuhusu namna nchi  hiyo ilivyoendelea katika masuala ya nishati ya Jotoardhi. Imetajwa kuwa nchi ya Iceland ni miongoni mwa nchi zilizoendelea katika nishati hiyo.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele akipata maelezo kuhusu masuala ya jotoardhi katika moja ya mabanda aliyoyatembelea mara baada ya kufungua Maonesho ya kuhusu masuala ya jotoardhi zikiwemo bidhaa na teknolojia zinazotumika katika nishati hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuendeleza Jotoardhi Tanzania, Mhandisi Boniface Njombe (wa kwanza kushoto mwanzo) akiongea jambo na baadhi ya wageni waliotembelea banda la Kampuni hiyo. Kampuni hiyo ya Jotoardhi ilianzishwa  mwaka 2014 .


Nishati ya Jotoardhi  inakua Afrika- Bilal

Makamu wa  Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal amesema ni wakati muafaka kwa Tanzania kuongeza vyanzo vya nishati ya umeme ikiwemo  vitokanavyo na nishati ya jotoardhi kutokana  na  umuhimu wake kwa maendeleo ya kiuchumi, vilevile kutokana  na Tanzania  kuwa  na hazina kubwa yenye viashiria vya jotoardhi.

Ameongeza kuwa,  nishati ya umeme ni miongoni mwa  maeneo ya
kipaumbele ya Serikali  kuhakikisha  taifa linakuwa na  nishati ya
kutosha ya umeme, ya uhakika na nafuu kutokana muhimu wa nishati hiyo
kwa maendeleo ya kiuchumi, kiviwanda na katika sekta ya kilimo na
kwamba ni chanzo cha nishati kisichokwisha.

Aidha, Makamu wa Rais amezitaka nchi wananchama zilizo katika bonde la
ufa na nchi nyingine  za Afrika kutumia fursa zinazotolewa na
Mashirika ya Kimataifa na Taasisi zilizobobea katika masuala ya
jotoardhi kuviendeleza vyanzo hivyo katika nchi zao kwa maendeleo ya
nchi hizo.

Kongamano hilo limefunguliwa leo tarehe 29 Oktoba, 2014 na
kuwashirikisha washiriki zaidi ya 400 kutoka nchi wananchama  kutoka
katika bonde la Ufa na nchi nyingine duniani, zikiwemo taasisi za
Kimataifa  zinazohusika na masusla ya jotoardhi na nchi nyingine
zilizopiga hatua katika nishati hiyo ikiwemo Iceland na litaendelea
hadi tarehe 31 Oktoba,2014.