(picha na Denis Mlowe)
Na Denis
Mlowe,Mufindi
KATIKA
kutekeleza maagizo ya Rais Jakaya Kikwete kila shule iwe na maabara tatu
ifikapo Novemba mwaka huu Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma (PSPSF) umetoa
msaada wa mabati 300 yenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni sita katika wilaya za
Kilolo na Mufindi, mkoani Iringa kufanikisha ujenzi wa maabara hizo na hosteli
kwa chuo cha Ualimu Mufindi.
Wakati
wilaya ya Kilolo imepata bati 200 zitakazotumika kusaidia kukamilisha ujenzi wa
maabara unaoendelea katika shule zake za sekondari, Chuo cha Ualimu
Mufundi(MUTCO) kilichopo mjini Mafinga wilayani Mufindi kimepata bati 100 ikiwa
ni kutumiza ahadi iliyotolewa na Meneja wa Sheria wa PSPF Abrahamu Siyovelwa
aliyotoa May 27 katika mahafali ya chuo hicho.
Akikabidhi
msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Mufindi Monica Kalalu juzi katika viwanja vya
Chuo cha Ualimu Mufindi(MUTCO) Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Iringa Baraka
Jumanne alisema lengo la msaada huo ni sehemu ya mpango wao katika kusaidia
sekta ya elimu nchini na kutekeleza maombi yaliyoombwa na viongozi wa wilaya hizo
katika kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete kila shule
ya sekondari iwe na maabara ifikapo Novemba mwaka huu.
"PSPF
ni shirika la mfuko wa pensheni hivyo faida lazima iifikie jamii hasa katika
suala la elimu ya za sekondari na msingi hivyo tumeamua kuwapatia mabati 100
chuo cha Mufindi na wilaya ya Kilolo mabati 200 kutekeleza maombi yao kwa
shirika la PSPF kusaidia ujenzi wa maabara na ujenzi wa hostel kwa chuo cha
Mutco hivyo leo tunawakabidhi madawati haya mia tatu kwa lengo la kutekeleza
ahadi ya shirika.” Alisema Jumanne.
Aidha
Jumanne alitoa wito kwa viongozi kuwashawishi wafanyakazi Kilolo na wanafunzi wa chuo cha Ualimu Mufindi kujiunga
mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma wa PSPF kwa huduma bora na mafao bora
yakiwemo mafao ya uzeeni,ulemavu,mirathi,mafao ya rambirambi za mazishi, malipo
ya wategemezi na malipo ya penshini ya kila mwezi.
Alitoa
faida ya kujiunga na PSPF kwa kuwa kuna baadhi ya mafao mbalimbali yanayotolewa
na mfuko huo yanalenga kuwawezesha
watumishi kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utumishi
wao kabla na baada ya kustaafu
Aliongeza
kuwa PSPF ina mpango imeweka mahususi wa kuhakikisha unaboresha maisha wa
wanachama wake wakiwemo wasio wafanyakazi kwa kuweka akiba isiyo ya hiyari
itakayowawezasha kufaidika kwa faida ya maisha yao.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Monica Kalalu alilishukuru shirika la
PSPF kwa msaada huo na kutoa wito kwa wanafunzi na walimu na kuwataka wadau
wengine wajitokeze kuisaidia sekta ya elimu hususani ujenzi wa maabara ambao
unaendelea nchi nzima kwa sasa
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerald Guninita alisema kuwa msaada huo utazisaidia
shule za sekondari za wilaya ya Kilolo katika kukamilisha ujenzi wa maabara na
kuwataka pspf wasiishie hapo katika kutoa msaada zaidi katika sekta ya elimu.
Na Amelia
Rweyimamu ambaye ni Muwakilishi wa PSPF makao makuu Dar es salaam, akizungumza
wakati wa kukabidhi bati hizo alisema kuwa PSPF inatambua umuhimu wa kuwepo kwa
maabara hapa nchini hivyo ofisi yake imeona vyema kushiri katika ujenzi huo kwa
kutoa bati hizo.
Rweyimamu
alisema PSPF inatoa mafao mbalimbali ikiwa ni pamoja na fao la uzeeni, fao la
ulemavu, fao la kifo, fao la mazishi, fao la wategemezi lisilo na kikomo, fao
la kujitoa, fao la uzee, fao la kufukuzwa kazi, na fao la ujasiriamali.
Aidha
aliongeza kuwa PSPF inatoa fao la elimu ambapo mfuko hudhamini mikopo katika
bodi ya mikopo ya wanafunzi, lengo kubwa ikiwa ni kujenga uwezo wa kuhudumia
wanafunzi wengi katika taaluma mbalimbali ikiwemo pia taaluma ya sayansi,
Teknolojia na Afya.