Waandaaji
wa Tamasha la Kiswahili Washington DC Ndugu Patrick Kajale na Dada
Finiana wakijadili jambo na ndugu Safari ambaye ndiye Mtunzi wa kile
kitabu Nambari moja Amazon cha Nyayo za Obama.
Afisa usalama wa ubalozi wa Tanzania Dr Mkama akiwa na baadhi ya maofisa wa ubalozi.
Maofisa wa ubalozi wakiendelea kula nyamachoma kutoka katika banda la Safari Restaurant DC
Nyama
Choma katika banda la Safari Restaurant Washington DC,Safari ni Mgahawa
wa Kitanzania uliopo katika jiji la Washington ambapo vyakula vingi
vya kinyumbani vinapatikana.
Mishikaki ikiendelea kuchomwa katika banda la Safari Restaurant kwenye Tamasha la Kiswahili
Watu wakiwa mstari kwenye banda la Safari wakijipatia nyama ya motomoto kutoka kwenye grill
Mabanda mbali mbali yakitangaza shughuli zao kwenye Tamasha la kiswahili
Miss Temeke- CEO wa Kwetu Fashion Design akiwa katika Meza yake baada ya kumaliza Maonyesho yake ya Mavazi ya Kitanzania.
Kwa mara
ya Kwanza kabisa nchini marekani limefanyka tamasha la Kiswahili katika
jiji la Washington, likijumuisha nchi zote za Afrika Mashariki na kati
zinazozungumza lugha ya kiswahili.Tamasha hili liliandaliwa ili kuweza
kutangaza tamaduni za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Chakula,
Mavazi, Ngoma za Asili, Miziki ya Kizazi Kipya,na mambo mbali mbali ya
kiasilia.
Waandaaji
Wanatoa Shukrani Kwa watu wote waliojitokeza kwani hii ni mara ya
kwanza kabisa Tamasha kama hili kufanyika nchini Marekani hivyo
tutegemee Mambo mengi Makubwa Mwakani kwani Huu ni Mwanzo.