 |
| Mashabiki
wa Mnadani Fc wakiwa wamembebe mchezaji wao Alawi Mohamed ambaye
aliwanyanyua mara mbili mashabiki hao toka vitini hatimaye ushindi
katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Pepsi kombe la Meya 214
dhidi ya timu ya Magazeti, hadi mwisho wa mchezo Mnadani Fc 2, Magazeti
1. |
 |
| Mpira
wa adhabu ukipigwa kuelekea langoni mwa timu ya Magazeti Fc, katika
mchezo wa robo fainali Pepsi kombe la Meya 2014, uliochezwa jana Uwanja
wa Nyamagana jijini Mwanza, Matokeo ya mchezo huo Mnadani Fc 2,
Magazeti 1. |
 |
| 'Mpira
uwekwe kati' kwa mujibu wa mwamuzi wa mchezo, mara baada ya goli la
kwanza la kusawazishwa na Mnadani Fc ikiwa ni dakika saba tu toka
Magazeti Fc walipopata goli la kuongoza, baadaye Mnadani Fc waliongeza
bao la pili na laushindi hivyo hadi mwisho wa mchezo Mnadani Fc
wakasonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa 2-1. |
Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 imefikia patamu, sasa ni katika hatua ya nusu fainali.
Timu zilitinga nusu fainali ya michuano hiyo ni:-
1.Sokoni FC
2.Mkolani
3.Mirongo pamoja na
4.Mnadani Fc.
Michezo
ya nusu fainali ya Pepsi Kombe la Meya 2014 itachezwa tarehe 17 na 18
mwezi huu ile hali fainali itakuwa jumamosi ya tarehe 20 katika Uwanja
wa Nyamagana jijini Mwanza.