Aisha Bui akiwa na Gabo katika moja ya scene...
AISHA Fathi ‘Aisha Bui’ anafunguka kwa kutamba kuwa
filamu yake mpya inayoingia sokoni siku ya jumatatu, itadhihiri kipaji
chake katika tasnia ya filamu, kwani amewakilisha wazo lake moja kwa
moja bila kupigwa alichoandika ingekuwa ni kazi ya kushirikishwa
isingekuwa rahisi.
Aisha Bui...
“Najua kila mtu anakuwa na uwezo wake katika filamu lakini unaweza
kushindwa kufanya hivyo kwa sababu ya kukosa nafasi ndio maana mimi
nimeamua kutumia kampuni yangu kutimiza ndoto zangu, wiki hii Yuneda
Entertainment wanasambaza kazi yangu mtaani,”anasema Aisha Bui.
Aisha Bui na Gabo wakipumzika baada ya kazi ngumu ya kushuti filamu hiyo.
Sinema hiyo ya Mshale wa Kifo inasambazwa na kampuni ya kizalendo ya
Yuneda Entertainment ya Jijini Dar es Salaam, ikiwa imetayarishwa na
Aisha Bui chini ya kampuni yake ya Badgirl Entertainment filamu yake ya
kwanza mwanadada huyu.

Filamu
ya Mshale wa Kifo inawakutanisha wasanii nyota wanaofanya vizuri katika
tasnia ya filamu Bongo kama vile Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Mzee
Korongo, Salim Ahmed ‘Gabo’, Aisha Bui na wasanii wengeine wakali, Aisha
anasema pia anazindua kampuni yake ya Badgirl Entertainment inayotoa
filamu ya Mshale wa Kifo.