Sep 5, 2014

Exclusive: MTV Base waongea kuhusu show wanayoshoot na Diamond


10632467_1525775407640577_1191827310_n
Kituo cha MTV Base jana kilikuwa kinazunguka na Diamond Platnumz kwenye mitaa mbalimbali jijini Johannesburg, Afrika Kusini kushoot kipindi chao kipya kitakachoanza kuonekana kwenye kituo hicho mwezi October mwaka huu. Tumewasiliana na uongozi wa kituo hicho nchini Afrika Kusini na hivi ndivyo ulivyotujibu:

“We were shooting the show yesterday with Diamond, and will be shooting again with him this afternoon. Basically it’s a 22 minute show following Diamond around while he’s in South Africa. The show will be released on air in October on MTV Base.”
10684286_326402764188366_2019991952_n
Katika show hiyo Diamond ataonekana pia akiwa ubalozi wa Tanzania nchini humo.
927772_289803997879926_2089105161_n
Katika hatua nyingine Diamond ametoa shukrani zake kwa mashabiki na watu wake wa karibu waliofanikisha kutajwa kuwania vipengele vinne kwenye tuzo za Channel O.
“Kwanza kabisa nitangulize shukran zangu nyingi kwa Media zote nje na ndani ya nchi… wadau na bila haswa kuwasahau nyinyi mashabiki zangu pendwa.. naamini nguvu na support zenu za kizalendo mnazozidi kunipa ndio zimepelekea kijana wenu leo kufikia hapa…… niwashUkuru pia @channeloafrica kwa fursa hii…. Africa! Ni muda wa Kupiga kura sasa.