Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi
wa Taasisi ya Vulcan ya nchini Marekani Bw. Dave Stewart (kushoto) na Bi. Lauren
Ryder, inayojihusisha na masuala ya kuidadi tembo katika nchi 18 barani
Afrika ikiwemo Tanzania, baada ya kufanya mazungumzo maalum ya ushirikiano
yaliyofanyika katika jiji la New York nchini Marekani jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Lazaro Nyalandu akiagana na
Bw. Dave Stewart kutoka Taasisi ya Vulcan inayojihusisha na masuala ya
kuidadi tembo katika nchi 18 barani Afrika ikiwemo Tanzania mara baada ya
kumaliza mazungumzo nao jana jijini
New York nchini Marekani.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Lazaro Nyalandu (watatu kulia)
akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Taasisi ya inaundwa
na Wanajeshi Wastaafu wa jeshi la Marekani walioanzisha umoja wao
ujulikanao kama (VETPAW)kwa ajili ya kusaidia Uhifadhi wa Wanyamapori
barani Afrika mara baada ya kumaliza mazungumzo baina yao jana jijini New
York, Marekani. Kushoto ni Balozi
wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi 