Mkurugenzi
wa Global Publishers, Eric Shigongo (katikati), ambaye kampuni yake
inaandaa tamasha hilo, akizungumza kwenye mkutano huo.
WASHIRIKI
wa ‘Tamasha la Usiku wa Matumaini’ leo wametambiana kwenye mkutano na
vyombo vya habari uliofanyika Hoteli ya Atriums iliyopo Sinza,
Afrika-Sana jijini Dar es Salaam.
Katika
mkutano huo wa tamasha hilo la burudani mabondia, Mada Maugo na Thomas
Mashali, kila mmoja amejitapa kumchakaza mwenzake katika pambano hilo
huku Mbunge wa Nzega, Dkt. Hamis Kigwangala, aliyewawakilisha wabunge wa
timu ya Simba alijitapa timu yake kuwamaliza Yanga.
Msanii
wa Filamu za Maigizo, Issa Mussa 'Clouds 112' ambaye katika tamasha
hilo atachapana makonde na Jacob Steven 'JB' katika mchezo wa 'boxing'
wote wameahidi kutifuana 'kinomanoma'.
Rais
na mwakilishi wa timu ya Bongo Muvi Unity, Steve Mengere 'Steve
Nyerere', alitamba timu yake kuigaragaza timu ya Bongo Fleva ambapo
mwakilishi wake, Haruni Kahena 'Inspector Haruni', alisema wao ndio
watakaoibuka kidedea na kuwapiga Bongo Muvi Unity kwa mabao 7-1 kama
walivyofanywa Wabrazil na Ujerumani wiki iliyopita kwenye nusu fainali
za Kombe la Dunia.
Tamasha
hilo linatarajiwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam, ambapo huu utakuwa ni mwaka wa tatu mfululizo
kufanyika likiandaliwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd.
(HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL. )
Mkutano ukiendelea.
Sehemu ya mapaparazi waliofika kwenye tukio hilo.
Rais
wa Chama cha Ngumi za Kulipwa nchini (T.P.B.O) Yasin Abdallah
(katikati) ambao ndiyo wasimamizi wa pambano la Maugo na Mashali katika
tamasha hilo, akizungumzia pambano hilo.
Meneja
Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (mwenye miwani) na
Mkurugenzi Chuo cha Uandishi wa Habari, Biashara na Utawala cha Mlimani
kilichopo Mbezi Kwa-Msuguri jijini Dar, Hassan Ngoma (kushoto kwa
Mrisho), wakifuatilia kinachoendelea.
Khalid Chokoraa wa Bendi ya Mapacha Watatu akifuatilia kinachoendelea.
Mwakilishi
na Rais wa Bongo Muvi Unity, Steve ‘Nyerere’, akielezea jinsi
watakavyowagaragaza wasanii wa Bongo Fleva kwenye pambano la soka.
Mwakilishi
wa timu ya Bongo Fleva, Inspector Haruni, akijibu mapigo kwa kueleza
jinsi watakavyowararua Bongo Muvi Unity. Kushoto ni mratibu wa tamasha
hilo, Luqman Maloto, na Eric Shigongo.
Bondia Mada Maugo akijitapa kumchapa mpinzani wake, Thomas Mashali 'Simba Asiyefugika'.
Mashali akimjibu Maugo na kujitapa kuendeleza kichapo.
Mbunge Hamisi Kigwangala anayeiwakilisha timu ya wabunge wa Simba akieleza jinsi walivyojiandaa kuwaadabisha wabunge wa Yanga.
Msanii
wa filamu, Jacob Steven 'JB', ambaye atachapana na msanii mwenzake,
Issa Mussa 'Clouds 112', akichimba mkwara jinsi atakavyomkalisha msanii
huyo.
Shigongo ‘akiwakutanisha’ mabondia wenye upinzani mkali, Mashali (kushoto) na Maugo (kulia).
Clouds
112 (kushoto) akimchimbia mkwara JB ambaye aliishia kumuangalia
kidharau na kusema anasubiri siku ya Agosti 8 katika Uwanja wa Taifa.
Sehemu ya wanahabari wakipata maelezo.