Kama ilivyokuwa kwenye tamasha hilo mwaka
jana ambapo Rais Kikwete alipuliza kipyenga kuashiria kuanza kwa
mtanange huo, waheshimiwa kibao wataoneshana uwezo wao dimbani kwa
kusakata kabumbu safi kumsaka mshindi.
Ukiachilia mbali gemu hiyo ya kipekee, kivutio kingine kitakuwa ni mechi ya soka kati ya Bongo Fleva na Bongo Muvi ambao nao watachuana vikali kumsaka mshindi.
NDONDI
Burudani nyingine itakayolipamba tamasha hilo ni ndondi ambapo mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali watavurumishiana makonde ulingoni kumtafuta mbabe, kwa upande wa wabunge, Mwigulu Nchemba atadundana na Hamis Kigwangala, Bongo Muvi, Jackob Steven ‘JB’ atazichapa na Issa Musa ‘Cloud 112’ na wengine wengi.
BURUDANI YA MUZIKIUkiachilia mbali gemu hiyo ya kipekee, kivutio kingine kitakuwa ni mechi ya soka kati ya Bongo Fleva na Bongo Muvi ambao nao watachuana vikali kumsaka mshindi.
NDONDI
Burudani nyingine itakayolipamba tamasha hilo ni ndondi ambapo mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali watavurumishiana makonde ulingoni kumtafuta mbabe, kwa upande wa wabunge, Mwigulu Nchemba atadundana na Hamis Kigwangala, Bongo Muvi, Jackob Steven ‘JB’ atazichapa na Issa Musa ‘Cloud 112’ na wengine wengi.
Mkali wa ngoma ya Johnny, Yemi Alade kutoka nchini Nigeria naye atatimba nchini kwa lengo moja tu, kukinukisha kwenye Tamasha la Matumaini. Listi ya wasanii wa Bongo ni ndefu wakiwemo Ali Kiba, Roma, Madee, Juma Nature na kruu nzima ya Wanaume Halisi, Madee na Wema Sepetu ambaye ameahidi kuimba na kucheza nyimbo za bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Tamasha la Usiku wa Matumaini linaletwa kwenu kwa udhamini mkubwa wa Vodacom, Azam TV, E. FM na Times FM, hii siyo ya kukosa!