Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Mkuu wa Chuo cha Sebastian Kolowa Memorial
University SEKOMU Askofu Dr.Stephen Munga(kushoto)Makamu Mkuu wa Chuo
cha SEKOMU Dr.Anneth Munga(watatu kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Chiku Galawa(kulia) wakikata utepe kuzindua rasmi ukumbi wa mihadhara wa
Benjamin William Mkapa wilayani Lushoto jana.(Picha na Freddy Maro)
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni muda mfupi
baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu chA Sebastian Kolowa Memorial
University mabapo alifungua ukumbi wa mihadhara na kuhutubia
wananchi.Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha SEKOMU Askofu Dr.Stephen Munga na
kulia ni makamu wa chuo Dr.Anneth Munga.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasililiza kwa makini wanafunzi kutoka
Irente school for the Blind wakati walipoimba shairi maalumu wakati wa
sherehe za ufunguzi wa ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa
katika chuo kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University SEKOMU jana.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanafunzi wa wageni waliohudhuria
sherehe ya ufunguzi wa ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa
uliofanyika katika chuo kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University
SEKOMU huko Lushoto Mkoani Tanga jana.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi
walihiudhuria mkutano wa Hadhara huko Bumbuli Wilayani Lushoto jana.