
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni
Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk. Mary Nagu
akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi
Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Nagu katika hotuba
yake,amesema atawasimamia Makatibu hao na kuhakikisha wanaanzisha Benki
yao ambayo itawawezesha kuweka abiba zao na kukopeshana pia.

Mgeni
Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania na Mshauri wa Mambo
ya Kisheria wa TAPSEA,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angela
Kairuki akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa Kongamano la nne la
Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Kairuki
amewahimiza Makatibu Muhtasi hao kuhakikisha wanaudumisha na kuulinda
umoja walionao,kwani umoja ndio msingi wa maendeo.

Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Pilli Mpenda akisoma hotuba yake kwenye ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 kwenye hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.


Washiriki wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania kutoka maeneo mbali mbali wakifatilia mada mbali mbali.
MC. Angella Bondo akiwajibika.
MC. Ephrahim Kibonde.

Washiriki wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania kutoka maeneo mbali mbali wakifatilia mada mbali mbali.
Picha ya pamoja na Watendaji wakuu wa TAPSEA.





























