“Mpango mzima utakuwa Agosti 8, mwaka huu ambapo historia itaandikwa upya pale Mabondia kama Mashali na Maugo wakizichapa ulingoni, pia ndondi kati ya Wabunge wanawake pamoja na mastaa wa kike wa Bongo Fleva.
“Kutakuwa na mechi ya kukata na shoka kati ya Wabunge wa Simba na Wabunge wa Yanga ambapo wataoneshana ubabe bila kusahau mastaa wengine kibao wa kutoka ndani na nje ya nchi watalipamba jukwaa kwa kuimba nyimbo zote kali, listi kamili ya washiriki itatoka, endelea kufuatilia hapahapa,” alisema Maloto.
Tamasha la Usiku wa Matumaini huandaliwa na Kampuni ya Global Publishers ambapo linachukuwa nafasi kila mwaka na hukutanisha mastaa wengi kwa pamoja na kusherehekea na kudumisha amani na upendo kwa Watanzania.

Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo akiongea jambo katika Tamasha la Matumaini la mwaka jana 2013.
Mwaka jana tamasha hilo lililifana hasusan pale wabunge wa viti
maalum, Halima Mdee na Ester Bulaya walipozipiga na wasanii wa Bongo
Movie, Jacqueline Wolper na Aunt Ezekiel.Mechi kali ya Bongo Fleva ikiongozwa na Jacob Steven ‘JB’ walichuana vilivyo na Wana-Bongo Fleva. Tamasha pia lilihudhuriwa na mastaa kibao wa ndani na nje ya Tanzania ambapo staa wa muziki Dk. Jose Chameleone aliliteka jukwaa kwa kupiga vibao vikali.
Kwa mwaka jana, mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, mwaka huu anatarajiwa kiongozi mwingine mkubwa wa nchi. Tusikikilizie