
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akifuatana na Mshauri wa Rais Uwekezaji Bw.Abrahman Mwinyi Jumbe
(kushoto) akipotembelea shamba la ufugaji wa samaki la kikundi cha
Hakiliki Mwambe kusini Pemba jana.

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akizungumza na Wananchi wa wanakikundi cha Ufugaji wa Samaki cha
Hakiliki Mwambe kusini Pemba jana,wa Pili (kulia) Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Abdilahi Jihadi Hassan

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akiteta na Watoto wa Kijiji cha Mwambe mara baada ya kuzungumza na
Wananchi wa wanakikundi cha Ufugaji wa Samaki cha Hakiliki
jana,alipofanya ziara katika Mkoa wa Kusini Pemba.

Wananchi
waumini wa Dini ya Kiislamu wa vijiji mbali mbali vya Mkoa wa Kusini
Pemba wakijumuika kwa pamoja katika futari iliyoandaliwa na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein,kwa wananchi hao katika viwanja vya Ikulu ya Chake Chake Pemba
jana.

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein (wa nne kulia) akijumuika na Viongozi na wananchi mbali mbali wa
mkoa wa Kusini Pemba katika futari aliyowaandalia jana katika viwanja
vya Ikulu ya Chake Chake

Baadhi
ya akinamama wa Mkoa wa kusini Pemba wakijumuika kwa pamoja katika
futari waliyoandaliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein
(hayupo pichani) katika Ukumbi wa Ikuu ya Chake chake jana, [Picha na
Ramadhan Othman,Pemba.]

Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa na Mkuu wa Wilaya ya
Chake chake Pemba Mwanajuma Majid katika futari iliyowaandalia wananchi
wa Vijiji mbali mbali vya mkoa wa Kusini Pemba hafla hiyo ilifanyika
jana katika ukumbi wa Ikulu ya Chake Chake.