Jun 17, 2014

WATOTO NJITI MAPACHA WATELEKEZWA NA BABA YAO, MAMA YAO AOMBA MSAADA

 Fatuma Hussein akiwa na watoto wake mapacha.

 Watoto mapacha wakiwa wamelalaWatoto mapacha wakiwa wamelala

 Rahma akiwa amelala usingizi mnono

Rahmu akiwa amepozi tu kiaina

DADA mmoja Fatuma Hussein (30), anaomba msaada kwa Watanzania baada ya kutelekezwa na mzazi mwenzake. Akizungumza na Global Publishers maeneo ya Magomeni Makanya, Dar dada huyo anadai kuwa aliishi na mzazi mwenzie kwa miezi miwili kama mke na mume na ndipo akapata ujauzito, wakati huo alishajitambulisha nyumbani kwao na kutoa posa baada ya kujifungua watoto  njiti mapacha wakiwa na miezi saba.

Anadai mzazi mwenzake aitwaye Mussa Unguja kamtelekaza, akaongeza kuwa huwa haji kuwaona watoto. “Nikimpigia simu hapokei lakini siku moja aliipokea na akasema hana shida na watoto wangu,  toka siku hiyo sijazungumza naye.

‘’Watanzania naomba msaada wa hali na mali, watoto wangu na wapenda na kwa sasa sina kazi, naishi kwa kubangaiza chumba chenyewe nimepanga,’’alisema Fatuma.

Kwa yeyote aliyeguswa na tatizo la dada huyu anaweza kuwasiliana naye kwa namba 0682 400 798, jina Fatuma Hussein.


Habari kwa hisani ya GlobalNews