Jun 20, 2014

LICHA YA KUFIWA NA BABA SEREY AICHEZEA TEMBO

Hisia kali: Kiungo wa Ivory Coast , Serey Die akilia wakati wimbo wa Taifa lake ukiimbwa.
MCHEZAJI wa kamataifa wa Ivory Coast , Serey Die ameonesha uzalendo kwa nchi yake baada ya kucheza  mechi ya kombe la dunia dhidi ya Colombia licha ya kufiwa na baba saa mbili kabla ya mchezo kuanza.
Kiungo huyo alimwaga machozi wakati wimbo wa taifa wa nchi yake ukiimbwa katika mchezo wa kundi C.
Wengi walijua pengine analia tu kwa kulipenda taifa lake, lakini kulingana na ripoti zinaeleza kuwa baba wa nyota huyo mwenye miaka 29 alifariki dunia muda mfupi kabla ya mechi kuanza mjini Brasilia.(A.I)