Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Saidi Meki Sadiki (katikati) akizungumza jambo wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili(MUHAS) lililo kwenye mpaka wa wilaya ya Kisarawe na mkoa wa Pwani leo.Wengine kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Bi.Therezia Mmbando,Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Bw. Archard Mutalemwa na Meneja wa Tanroad mkoa wa Dar es salaam Bw. Ndyamukana Julius
Mkazi wa eneo la Mloganzila Bw. Fredy Justine Masondole (Katikati) akiwapeleka katika eneo la nyumba yake lenye mgogoro viongozi wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meki Sadiki (upande wa nyuma katikati), mkuu wa wilaya ya Kinondoni Jordan Lugmbana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbando.
Mafudi wakiendelea na ujenzi wa awali wa ofisi za muda katika eneo itakapojengwa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili(MUHAS) lililo kwenye mpaka wa wilaya ya Kisarawe na mkoa wa Pwani leo
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Saidi Meki Sadiki (kushoto) akizungumza na mkazi wa eneo la Mloganzila Bw. Fredy Justine Masondole (kulia) ambaye aliweka pingamizi kuzuia miundombinu ya maji, umeme na barabara kupita katika eneo lake , Hata hivyo mkazi huyo aliruhusu ujenzi kuendelea baada ya mazungumzo ya kupatikana kwa muafaka kufikiwa. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Felchian Mramba.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
