Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Akash.
Mkurugenzi Mkuu wa Teknolojia, Nyangu Meghji (katikati) akielezea maboresho yaliyofanywa na Raha katika huduma za internet.
KAMPUNI inayotoa huduma za internet nchini, Raha, imepanua wigo wa mawasiliano katika internet kwa kutumia teknolojia za 4G WiMax Solution pamoja na Fiber Optic.
Raha kwa sasa wanatoa huduma za internet katika mikoa mbalimbali nje ya Dar es Salaam ikiwemo Tanga na Arusha kwa kutumia teknolojia ya rahaSpots ambayo inamuwezesha mteja kupata huduma bora popote alipo.
Kwa maboresho haya, Raha wanawaahidi huduma bora zaidi wateja wake ikiwemo kuperuzi kwa haraka mitandao mbalimbali ya kijamii na tovuti.
PICHA / HABARI: DENIS MTIMA