Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Mkurugenzi wa hifadhi ya jamii wa PPF Kanda ya Ziwa Meshark Bandawe ambapo ni moja kati ya wawekezaji ndani ya benki hiyo
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiweka jiwe la msingi la Benki ya Azania Tawi la Lamadi huku akishuhudiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Azania Bwana William Erio (wa pili kushoto)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Azania Bwana William Erio(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bwana Charles Singili (kulia) wakifurahia hatua ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa uzinduzi wa Benki ya Azania Tawi la Lamadi
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi walio ndani ya Benki kuhakikisha kuwa huduma inatolewa kwa kuwango.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia amewataka wananchi wa Lamadi mkoani Simiyu kujinufaisha kwa kuzichangamkia fursa za uwekezaji zilizomo ndani ya Benki ya Azania kama zifanyavyo taasisi nyingine kubwa za kitanzania.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Azania Bwana William Erio(wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bwana Charles Singili(kushoto) wakikata utepe kuzindua rasmi Benki ya Azania Tawi la Lamadi jana. Kulia nia mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti.












