Kikao cha Kamati Kuu ndiyo kimeisha muda huu, na taarifa zilizopo ni kwamba kambi ya PM7 imevunjwa rasmi baada ya viongozi wake kuvuliwa vyeo vyote walivyo navyo ndani ya chama.
Waliovuliwa vyeo ni Zitto Kabwe, ambaye amevuliwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa chama pamoja na nafasi ya Naibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Dr. Kitila Mkumbo yeye amevuliwa nafasi ya mjumbe wa kamati kuu.
Kamati Kuu imewaandikia barua Zitto na Kitila, wajieleze ndani ya siku 14 kwanini wasifukuzwe uanachama.
Tunawapongeza kamati kuu kwa hatua hii muhimu kwa mustakbali wa chama na taifa
Peopleeeezzzz!!!!
sababu za zitto kabwe kuvuliwa uongozi hizi hapa
Quote By tamuchungu View Post
1. maono yake kugombea uenyekiti wa chadema na siku moja agombee urais
2. kukataa posho za vikao bungeni na hivyo kuingilia maslahi ya wabunge wenzake.
3.kuhoji mapato na matumizi ndani ya vyama hususan ruzuku inayotolewa na serikali.
4eneo analotoka, kwamba hatoki eneo ambalo ni strong hold ya chama chake.
je masuala haya yamefikia kiwango na uzito kwa mwanasiasa huyu kijana kufanyiwa aliyofanyiwa??
