Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Lupando,Kata ya Masoko Wilayani Rungwe mapema leo,Kinana alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kutatua tatizo sugu la Maji na Barabara katika kijiji hicho,alichozaliwa Mbunge wa jimbo la Rungwe Magharibi,Mh.Dkt David Mwakyusa.Aidha kinana aliitahadharisha Serikali katika suala zima la kuitaka Serikali iache urasimu na umangimeza katika mipango ya maendeleo kwa Wananchi,kwa sababu Urasimu na umangimeza huo huwanufaisha zaidi wanaoshikilia fedha za miradi hiyo wakati wananchi Wanaumia na kuteseka kwa kukosa huduma muhimu mbalimbali
Pichani shoto ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,Dkt Mary Mwanjelwa akiwa na Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya kimataifa,Dkt Asharose Migiro walipokuwa wakielekea kukagua jengo la bweni la kulala wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ikuti,Wiayani Rungwe mkoani mbeya leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kujenga moja ya nyumba ya waalimu katika shule ya sekondari ya Ikuti iliopo katika kata ya Ikuti,Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya mapema leo,akiwa sambamba na Ujumbe wake hawapo pichan,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Asharose Migiro.Kinana na Ujumbe wake wako ziarani Wilayani Rungwe Magharibi mkoani Mbeya,ambapo kesho watakuwa wilaya ya Ileje kutekeleza Ilani ya chama,kukagua miradi ya chama na wanachi sambamba na kujua na kutatua matatizo yao kwa namna moja ama nyingine.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
