Picha juu na chini ni baadhi ya wakinamama wa Chalinze wakifuatilia mafunzo hayo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki
Mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba akikabidhi vyeti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo.
Picha juu na chini mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba na Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude Sima wakiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu.
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude Sima (kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba (kulia) kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya siku sita kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira rasmi na wanaoishi pembezoni katika juhudi za kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
.Zaidi ya wanawake 220 wafikiwa na mradi huo wa Shirika la Kazi Duniani
Na Damas Makangale, Chalinze Moblog.
SHIRIKA LA KAZI DUNIANI (ILO) limeendesha mafunzo ya siku sita kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira rasmi na wanaoishi pembezoni katika juhudi za kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi. Moblog inaripoti. Mradi huo wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unalenga wanawake wote ambao wapo pembezoni wa barabara na mipakani kwa sababu wapo katika hali ya hatarishi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa Pwani Wilayani Chalinze, Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Getrude Sima amesema ndani ya siku sita mradi wa mapambano ya Ukimwi chini ya ILO umewafikia wanawake 120 katika kata za Pera, Chamakweza, Mpingo, Bwilingu, Msolwa na Mdaula
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
