Wastara amefichua siri kwamba
kioo ndicho kilisababisha aanzishe uhusiano wa mapenzi na marehemu Juma
Issa Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki Januari 2, mwaka huu.
Wastara aliweka bayana kuwa
marehemu Sajuki ambaye alikuwa mumewe, hakuwahi kumtongoza lakini kioo
ndiyo kilikuwa chanzo kilichosababisha wajikute wameingia dhambini kwa
mara ya kwanza.
Akizungumza na gpl, Wastara alisema
kuwa siku hiyo walikuwa wakifanya mazoezi ya filamu moja (hakutaja
jina) nyumbani kwake na Sajuki alikuwa muongozaji wa sinema hiyo.
“Ilikuwa ni usiku wa manane tukiwa
nyumbani kwangu tukifanya mazoezi ya filamu moja, sasa ilikuwa ni scene
ya mapenzi tukawa mbele ya kioo huku tumekumbatiana.
“Tukaendelea hivyoo, mmh! Sasa
tulivyokitazama, tukahisi tunaendana. Tukaendelea kujifanyia tathmini na
ghafla tukajikuta tunafanya kweli, kioo kilisababisha tukajikuta
tunafanya mapenzi,” alisema Wastara kwa uso wa aibu
