askari wakiwa katika eneo la tukio baada ya mauaji kufanyika
wananchi wakiwa katika tukio kushudia
mwili wa marehemu akie jifanya mwehu na kuanza kumchoma visu mwilini mwenzake hapa akiwa amekwishapotezmaisha
Huyu ndiye marehemu kijana maarufu kwa jina la 'Mkandarasi'
anayesadikika kufanya mauaji kwa mumchoma kijana mwenzake kisu naye
aliuawa na wananchi wenye hasira katika mtaa wa Msikiti wa Ijumaa jijini
Mwanza.
Watu wawili wameuawa katika tukio la utata lililotokea jana asubuhi
majira ya saa 3 na dakika kadhaa, katika eneo la barabara ya msikiti wa
Ijumaa jijini Mwanza.
anayesadikika kufanya mauaji kwa mumchoma kijana mwenzake kisu naye
aliuawa na wananchi wenye hasira katika mtaa wa Msikiti wa Ijumaa jijini
Mwanza.
Watu wawili wameuawa katika tukio la utata lililotokea jana asubuhi
majira ya saa 3 na dakika kadhaa, katika eneo la barabara ya msikiti wa
Ijumaa jijini Mwanza.
hapa ni eneo la msikiti wa ijumaa ambapo ndipo yalipofanyika mauaji haya kutisha
raia wakiwa juu ya gorofa wakishuhudia mauaji hayo
Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa kilisababishwa na kijana mmoja
maarufu kwa jina la Mkandarasi kumchoma kisu kijana mwenzake ambaye
alikuwa mgeni akifanya kazi za usaidizi kwa mamantilie wanaopika chakula
katika moja ya viunga vya ndani eneo la vichochoro vya mtaa wa Msikiti
wa Ijumaa kufuatia majibizano ambayo yalisababisha kijana Maarufu kwa
jina la 'Mkandarasi' amchome mwenzake kisu cha shingoni na sehemu
nyingine za mwili.
Kijana huyo alipoona amezidiwa alitafuta upenyo na kukimbia huku damu
zikimchirizika, hata hivyo hakufika mbali kwani alizidiwa na hatua
chache baadaye alianguka chini nakuaga dunia Wananchi wenye hasira walimzingira muuaji ambaye naye alikuwa akijihami
kwa kisu alichokuwa nacho mkononi na ndipo walipofanikiwa kumbwaga chini
na kumshambulia kwa mawe hadi umauti.
Akisimulia juu ya mkasa huo mmoja kati ya mashuhuda Peter Nyamoko
anahadhithia. (Msikilize hapa chini)
Naye ndugu wa marehemu aliyeuawa kwa kuchomwa kisu alipohojiwa alikuwa
na haya machache. (Msikilize hapa chini)
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linataraji kuja na taarifa kamili ya
Uchunguzi wake hii leo.






