Baada ya siku ya jana kupatikana kwa
habari za Dogo Janja kutimuliwa kundi la Watanashati Entertinment lililo
chini ya uongozi wa Ostaz Juma Namusoma kwa utovu wa nidhamu na tabia
mbaya ambayo dogo Janja alikuwa ameianzisha. Tofauti na wengi
walivyodhani kuwa Dogo Janja atarudi kwa Arusha na maisha yatasonga
lakini imekuwa sivyo, Dogo janja alielwa kosa lake na kuamua kuomba
msamaha katika Uongozi wa Watanashati na kukubaliwa na kurudi kundini
kama zamani, Mtoto akinyea mkono huwezi kuukata ila utaosha na maisha
yataendelea kama kawaida, hii ndiyo falsafa aliyoitumia Ostaz Juma
Namusoma kwani anamchukulia Dogo Janja kama mwanae au mtu wake wa karibu
Akizungumza na Mtandao huu, kiongozi wa Mtanashati Entertainment Ustaadh Juma Namusoma alisema kuwa sababu za kumtimua Dogo Janja ni utovu wa nidhamu, unywaji pombe, kutokwenda shule pamoja na uvutaji bangi. Aliongeza kuwa tayari amempatia nauli ya shilingi 90,000/= kurudi nyumbani kwao jijini Arusha alipotokea. Dogo Janja alitua kwa mbwembwe jijini Dar es Salaam kwa ndege Juni 22 mwaka jana akitokea Arusha