Sep 28, 2013

HIVI NDIO SEMINA YA FURSA ILIYOFANYI NDANI YA UKUMBI WA GOLDCREST HOTEL JIJINI MWANZA: WANANCHI WAFUNGUKA KUTAKA KUIPATA ELIMU JUU YA FURSA ZA MAISHA

hii ndio meza kuu ya wadau wa semina ya fursa  iliyo fanyika jijini mwanza ukumbi wa goldcrest hotel


Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele (mwenye miwani) akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB),Bi.Magreth Chacha walipokuwa wakiwasili kwenye  semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii,pichani kati ni Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group,Bwa.Ruge Mutahaba.











Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika semina hiyo

Mmoja wa waigizaji mahiri wa filamu hapa nchini Elizabeth Michael akijulikana zaidi kwa la kisanii kama Lulu akiwasili kwenye semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii,ambapo pia atazungumzia mambo kadhaa mbalimbali kwenye semina hiyo,ambayo itawakutanisha Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba,Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini na watoa mada wengine mbalimbali.


 Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akizungumza mada iliyohusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nishati na madini ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu,iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Gold Crest.






 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Maxcom inayouza bidhaa yake ijulikanayo kama Max Malipo,Bwa.Juma Rajab akizungumzia kuhusiana na fursa ya bidhaa yake ya Max Malipo inavyoweza kuisadia jamii kwa namna moja ama nyingine.
Mmoja wa wasanii wa bongofleva,Nikki Wa Pili akizungumza kwenye semina ya kamata fursa twendzetu.

 Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida,Mh.Yahaya Nawanda akizungumzia mada yake iliyohusu suala la ufugaji,hasa kuku wilayani mwake

Hizi ni picha za jinsi semina ya fursa ilivyoenda leo 28/9 mchana. Kulikuwa na wazungumzaji mbalimbali kama Lulu,Mr Sebastian Maganga,Mr Ruge Mutahaba, Nikki wa Pili na wengine wengi. Cheki jinsi watu wangu wa Mwanza walivyopata darasa la fursa

Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba akizungumza 
na wadau wa kupata elimu hiyo ya bure kabisa